VIDEO: Mashabiki Simba wafurika

Tuesday February 12 2019

 

By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Katika mechi ya Simba na Al Ahly Ligi ya Mabingwa Afrika, mashabiki wa Msimbazi walionekana kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Pengine katika hali ambayo haikutegemewa baada ya kikosi hicho kukubali kufungwa mabao kumi katika mechi mbili za ugenini katika ligi hiyo. Mashabiki wa Simba walikuwa wengi na kwa muonekano wa kawaida walionekana waliujaza uwanja kwa lengo la kupangua nguvu ya wapinzani wao.

 Huenda mashabiki hao walijitokeza kwa wingi kutokana na kauli ambayo ilitolewa na mdhamini wao Mohammed Dewji 'MO'. Wiki iliyopita katika mkutano na waandishi wa habari MO aliwaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi na kusahau matokeo ya mechi zilizopita.

MO mwenyewe alijitokeza uwanjani kushuhudia timu yake ikimaliza kipindi cha kwanza ikishindwa kugusa nyavu za Al Ahly.

Advertisement