VIDEO: Dito afichua siri ya mafanikio aliyowaachia Ruge THT

Monday March 4 2019

By Rhobi Chacha

Msanii wa muziki kutoka THT Dito ,amesoma salamu kutoka THT kwenye kumuaga Ruge Mutahaba mkoani Kagera leo Jumatatu.

Dito amesoma salamu hizo kwa niaba ya kundi la THT,ambapo amesema, Ruge alikuwa mtu muhimu sana na hata ulipokuwa ukimkosea sana  alikuwa hakati tamaa.

Amesema alikuwa mtu ambaye wa kusamehe na kuanza maisha mapya na kutupa muda wa kusimamia kazi zetu na kujipanga upya.

Aidha amesema kauli waliyoachiwa na Ruge anasema alikuwa anapenda kuwaambia kuwa kuishi kwa usawa na kupambana ,heshima kwa watu wote.

Advertisement