Uwanja wa nyasi asili Simba SC usipime kabisa

Muktasari:

Katika uwanja huo walionekana wanamama wakiwa wanatoa nyasi zilizojifunga funga kwa kuzikata kwa umakini.

Dar es Salaam.Achana na nyasi za bandia, klabu ya Simba SC imekamilisha uwanja wake wa nyasi za asili katika eneo lao la Uwanja wa Bunju.

Mwanaspoti imefika uwanjani hapo na kushuhudia nyasi za bandia zikiwekwa, pia upande wa uwanja wa nyasi za asili ulikuwa kati hali ya juu.

Katika uwanja huo walionekana wanamama wakiwa wanatoa nyasi zilizojifunga funga kwa kuzikata kwa umakini.

Kwa upande mwingine umwagiliaji katika uwanja huo ulikuwa mkubwa wakitumia vifaa maalumu pamoja na mpira ambao ulikuwa ukirahisisha umwagiliaji wa maji katika nyasi hizo.

Hali ya rangi iliyopo uwanjani hapa ni kijani ya kuvutia huku nyasi zake zikionekana kuwa na ukijani wa kutosha.

Katika upande mwingine eneo la pembeni ambalo watakuwa wanatembea watu kwa miguu, eneo hilo wameweka vigae vilivyopangwa vizuri.