Unai Emery hashikiki hadi Europa

Muktasari:

Arsenal, Chelsea, Lazio zimefuzu kucheza hatua ya makundi ya Europa Ligi, huku kocha Emery akipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo msimu huu

LONDON, England. MWANGA wa nani atasonga mbele katika mechi za LEuropa League umeanza kuoneka kwa baadhi ya timu huku Arsenal ikitakata kwa kucheza mechi yake ya 11 bila kupoteza kwa mashindano yote.
Katika mechi za juzi usiku, mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud amemaliza ukame wa mabao alipoifungia timu yake bao pekee wakati  Chelsea ilipoilaza BATE Borisov na kukata tiketi ya hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo huku ikiwa na mechi mbili mkononi.
Giroud hajaifungia Chelsea kwa miezi sita lakini akamaliza ukame wake juzi usiku dhidi ya BATE. Msimu uliopita, mchezaji huyo aliyekuwa Arsenal alicheza mechi mbili za timu hiyo Ligi ya Europa.
Wakati Chelsea ikifanya mambo yake, Arsenal nayo ilikata tiketi baada ya suluhu na Sporting katika mchezo ambao mchezaji wake, Danny Welbeck aliumia vibaya kiasi cha kuwahishwa hospitali.
Mshambuliaji huyo wa England alilazimika kuchukuliwa kwenye machela baada ya kuumia enka hatua ambayo pia ililazimika mchezaji huyo kuwekewa oksijeni kabla ya kupelekwa hospitali.
Klabu ya Zurich nayo ilifuzu pamoja na Bayer Leverkusen ambayo ilishinda bao 1-0. Eintracht Frankfurt iliifunga Apollon Limassol 3-2 na kusonga mbele, wakati Lazio iliichapa Marseille 2-1 na kuingia raundi inayofuata.
Mambo yakazidi kunoga kwa Dinamo Zagreb ilikata tiketi ya kusonga mbele baada ya kufanya vyema kwenye mechi zake nne. Ikicheza na watu 10 uwnajani, Sevilla ilishinda mabao 3-2 mjini Akhisar kwa penalti ya dakika za alasalama na kumaliza kabisa matumaini ya Anderlecht’s kusonga mbele.

CHELSEA v BATE
Emerson Palmieri alinyunyiza krosi dakika ya 53 na Giroud akauendea hewani na kuandika bao kwa Chelsea. Mchezaji huyo alisimama mbele dhidi ya BATE badala ya Alvaro Morata aliyekuwa amepumzishwa.
‘Amenifurahisha,” alisema kocha wake, Maurizio Sarri akiongeza: " Giroud ni mchezaji muhimu sana kwetu, anatumika vizuri, anajua vizuri kwamba wakati gani anataka kufunga na anajiamini.
“BATE wamechweza vizuri. Hawakuwa tu na bahati kwani wangeweza kutoka hata sare.”
Chelsea sasa iko kileleni mwa Kundi L ikiwa na pointi 12. Timu ya Hungary ya Vidi ni ya pili ikiwa na pointi sita baada ya ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya PAOK .

ARSENAL YABANWA
Arsenal imebanwa mbavu na kutoka suluhu na Sporting, huku Jeremy Mathieu kwa kumchezea rafu mbaya Pierre-Emerick Aubameyang dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.
Aubameyang, aliyeingia badala ya Welbeck dakika ya 30, alipoteza nafasi nyingi za kufunga.
Arsenal iko kileleni mwa Kundi E ikifikisha pointi 10, ikiwa na pointi tatu zaidi ya Sporting. Qarabag inaungana na Vorskla kwa kuzoa pointi baada ya ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya timu hiyo.

BETIS
Miamba ya Hispania ikiongozwa na kiungo wake, Suso alitandika mkwaju mmoja matata na kuisawazishia timu yake na kufanya matokeo kuwa 1-1 huku mabingwa mara saba,  AC Milan ilikuwa na Real Betis, ambayo ilipata bao lake kupitia kwa Giovani Lo Celso.
Betis sasa iko kileleni mwa Kundi F ikiwa na pointi nane, pointi moja zaidi ya Milan ikifuatiwa na Olympiacos iliyoichakaza Dudelange mabao 5-1.

SEVILLA
Ever Banega wa Sevilla alifunga penalti dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho na kuibuka na ushindi dhidi ya Akhisar katika mfululizo wa michuano hiyo.
Mapema, Nolito na Luis Muriel waliipa miamba hiyo ya Hispania ushindi wa mabao 2-0 lakini Elvis Manu alianza kuifungia Akhisar dakika ya  52 na dakika nne baadaye Sergi Gomez alitolewa nje kwa kulimwa kadi nyekundu. Onur Ayik akiwasawazisghia waturuki hao dakika ya 78.

Sevilla iko juu Kundi J ikiwa na pointi tisa ikifungana na Krasnodar ya Russia ambayo nayo iliilaza Standard Liege mabao 2-1.

MAKUNDI MENGINE
Takumi Minamino aliifungia hat-trick Salzburg ikiibuka na ushindi wa mabao 5-2 mchezo uliopigwa Rosenborg. Huo ni mchezo wa nne kushinda kutok Kundi hilo la B. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Celtic iliikandamiza Leipzig 2-1 na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi sita.
Kundi H, Luka Jovic, Sebastien Haller na Mijat Gacinovic walifunga wakati Eintracht ikifanya mauaji hayo kabla ya Emilio Zelaya kuifungia Apollon, na mabao yote ni kwa mikwaju ya penalti.
Eintracht imefikisha pointi 12 ikifuatiwa na Lazio yenye pointi 10. Marseille na Apollon, zina pointi moja na zimeshatolewa.
Kundi G, Spartak Moscow iliilaza Rangers 4-3 ikitokea nyuma baada ya kutangulia kufungwa 3-2. Villarreal ndiyo inayoongoza ikiwa na pointi sita baada ya suluhu na Rapid Vienna. Rangers na Spartak zina pointi moja kila mmoja.
Anderlecht imeaga michuano hiyo kwa kipigo cha mabao 2-0 mechi ya Kundi D dhidi ya Fenerbahce. Zagreb yenyewe imefuzu baada ya kuishinda mabao 3-1 Spartak Trnava.