Unaambiwa Welbeck anaakipona tu moto uleule

Muktasari:

 

  • Welbeck hata hivyo, hatarajiwi kwa sasa kurudi msimu huu lakini matarajio ni kurudi upya baada ya kupona kabisa.

London, England .MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Danny Welbeck ameahidi atarudi kwa nguvu zote akiwa timu huku akiwashukuriu mashabiki wa klabu yake kwa kumpa nguvu kipindi hiki anachouguza enka yake aliyofanyiwa upasuaji.

Mchezaji huyo alianguka dakika ya 30 katika mchezo dhidi ya Sporting Lisbon ikiwa ni mfululizo wa michuano ya Europa League na kulazimika kuwekewa msaada wa hewa ya oksijeni, mpambano huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Emirates.

Arsenal ilithibitisha kuwa Welbeck anaendelea vizuri na kwamba anataraji atakuwa vizuri.

Welbeck hata hivyo, hatarajiwi kwa sasa kurudi msimu huu lakini matarajio ni kurudi upya baada ya kupona kabisa.

Mshambuliaji huyo aliwapongeza mashabiki wake kwa kumtumia ujumbe wa kutakia kila la kheri na akasema anawashukuru wote kwa kumuunga mkono na upendo.

‘Hakuna shaka nitakuwa vizuri na nitarudi mwenye nguvu zaidi. Naona mambo yanaanza sasa. Najua nitarudi nikiwa niko imara.’

Bernd Leno alisema kwamba kocha Unai Emery aliwaambia wachezaji wote wa Arsenal kwenda kumuona  Welbeck kabla ya mchezo wa Arsenal na Wolves.

‘Nafikiri alifurahi sana kutuona. Welbeck ni sehemu ya timu na tutamsapoti kwa hali na mali,’ Leno alisema. ‘Ni suala la kuwa na subira na ukweli tunamkosa na Danny tunamuhitaji kwa ajili ya ushindi.