Tammy kafunika wengine Chelsea

Muktasari:

Staa Giroud kwenye kikosi cha Chelsea msimu uliopita alicheza mechi 45 na kufunga mabao 13. Kwa rekodi hizo unaweza kuona bayana kwanini Lampard anampendelea Tammy kwenye fowadi yake, anafunga.

LONDON,ENGLAND.MASHABIKI wa Chelsea wanapambana kumtaka kocha Frank Lampard aanze kuwaanzisha Michy Batshuayi kwenye fowadi baada ya kuona Tammy Abraham na Olivier Giroud wamechemsha, na kushindwa kuisaidia timu hiyo kufunga.

Hata hivyo, mashabiki hao wamesema hivyo bila ya kutazama rekodi za washambuliaji hao watatu, ambapo kwa Tammy, katika mechi 40 alizocheza kikosi cha Aston Villa alikokuwa kwa mkopo msimu uliopita amefunga mabao 26, huku Batshuay alicheza kwa mkopo Crystal Palace mechi 13 na kufunga mabao sita, wakati mkopo wake huko Valencia mechi 23 alifunga mara tatu.

Staa Giroud kwenye kikosi cha Chelsea msimu uliopita alicheza mechi 45 na kufunga mabao 13. Kwa rekodi hizo unaweza kuona bayana kwanini Lampard anampendelea Tammy kwenye fowadi yake, anafunga.