Straika Mbaraka Yusuf arejea tena kuongeza makali Azam FC

Thursday May 16 2019

 

By Charity James

BAADA ya kufanikiwa kuipandisha daraja klabu ya Namungo FC, mshamuliaji Mbaraka Yusuf anatarajia kurejesha makali yake katika timu yake ya zamani ya Azam FC.

Sia Mbaraka tu ambaye anatarajia kurudi klabuni hapo baada ya kutolewa kwa mkopo nyota wengine ni kipa Matacha Mnate, Abdul Haji, Hami karim wote walikuwa kwa mkopo Mbao FC, Abdallah Masoud, Ismail Gambo, Braison Paphael (KMC), Sawalehe Abdallah Afrika Lyon.

Wengine ni Wazir Junior Biashara United, Ditram Nchimbi Mwadui fc, Ramadhani Mohammed Reha FC na Oscar Masai ambaye alikuwa na Mbaraka Namungo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mratibu wa Azam FC, Philip Alando alisema nyota hao wote wanarudi katika klabu yao hiyo ya zamani kwani waliondoka kwa makubaliano ya msimu mmoja.

Alisema wachezaji wao wengi wanapowatoa kwa mikopo inakuwa ni msimu mmoja mmoja na baadaye wanarudi tena klabuni na kuweka wazi kuwa uamuzi wa kuwatumia kikosini au kutokuwatumia utatolewa na mwalimu.

"Wachezaji hao niliokutajia wote wanamikataba na Azam FC tuliwatoa kwa mkopo kwenda kuongeza viwango kwenye klabu nyingine kwa muda wa msimu mmoja mmoja msimu huu ukiisha wanarudishwa mwalimu atajua nani atabakinae kikosini kwake na nani atamtoa tena kwa mkopo," alisema.

 

Advertisement