Stonetown yabeba ndoo

Saturday August 10 2019

 

By Salim Hamad ,Pemba

TIMU ya Stone Town Zanzibar, imetawazwa mabingwa wa mchezo Kikapu baada ya kuichakaza Nyuki kwa 50-45 mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Tenisi Chake Chake.
Katika mashindano hayo, KVZ ikanyakulia ubingwa kwa upande wa wanawake huku JKU ikachukua nafasi ya pili.
Akizungumza mara baada kumalizika michuano hiyo Ofisa Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo, Fatma Hamad Rajab alisema Serikali  itahakikisha inaondoa changamoto zinazoikabili michuano hiyo ikiwemo kuboresha Viwanja.
Alisema tayari serikali inatambua michezo hiyo inakabiliwa na changamoto za Uwanja hiyo itajitahidi kuona changamoto hiyo inaondoka.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Kikapu Zanzibar, Mwanache Khamisi ameviomba vyombo vya Ulinzi na Usalama kisiwani hapa kuanzisha michezo hiyo na kuifanya kuwa endelevu kwani inasaidia kukuza vipaji na mashirikiano.

Advertisement