Stars yaiwahi Guinea ya Ikweta mapemaa

Friday November 8 2019

 

By Charity James

KATIKA kuhakikisha wanapata matokeo mazuri nyumbani kwenye mchezo wao wa kwanza wa kuwania Fainali za Afcon 2021, kikodi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinatarajiwa kuingia kambini kesho Jumamosi ili kujiandaa dhidi ya Guinea ya Ikweta katika mechi za makundi.
Vijana hao wa Etienne Ndayiragije kinasaka tiketi ya kwenda tena katika fainali hizo za Afrika kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo 1980 nchini Nigeria na mwaka huu zilipofanyikia Misri.
Fainali hizo za mwakani zitafanyika Cameroon na Stars imepangwa kundi moja la J na Guinea ya Ikweta, Libya na Tunisia.
Ndayiragije amewaita wachezaji 27 kwa maandalizi ya mchezo huo wa kwanza utakaopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam Ijumaa ijayo ikiwa wiki kadhaa tangu watinge fainali za CHAn 2020 zitakazofanyikia pia Cameroon mwakani.
Akizungumza na Mwanaspoti, Ndayiragije alisema anatarajia kuwasiri nchini kesho kutokea Bunjumbura tayari kwaajili ya kuanza kukinoa kikosi hicho ili kiweze kufikia mafanikio.
"Leo usiku wachezaji wengi walioitwa katika kikosi wanahitimisha michezo yao ya ligi hivyo kesho mapema wataanza kuingia kambini mdogo mdogo hadi watakapokamilika wote," alisema.
"Yanga wanacheza Mtwara leo, KMC pia wanamchezo lakini Azam ndio wanamaliza usiku hivyo watatakiwa kuingia kambini mapema ili tuweze kuanza maandalizi lengo ni kuona timu inafanya vizuri na kupata nafasi ya kuingia hatua inayofuata," alisema.
Nyota walioitwa kwenye kikosi hicho ni Juma Kaseja, Metacha Mnata, David Kisu, Salum Kimenya, Ramadhan Kessy, Mohamed Hussein, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Bakari Nondo, Kelvin Yondan, Dickson Job, Jonas Mkude, Abdul-azizi Makame, Saimon Msuva.
Wengine ni Eliuta Mpepi, Iddi Seleman, Salum Abubakar, Ditram Nchimbi, Shaban Idd, Mzamiru Yassin, Frank Domayo, Mbwana Samatta, Farid Mussa, Miraji Athuman, Hassan Dillunga, kelvin John na Ayub Lyanga.

Advertisement