Stars kujipima nguvu na Misri

Muktasari:

Misri ambao ni wenyeji wa mashindano hayo mwaka huu, wapo kundi A pamoja na timu za DR Congo, Uganda na Zimbabwe.

Story Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri kama sehemu ya maandalizi yake kuelekea Fainali za Mataifa ya Afrika zitakazochezwa nchini Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Juni 13 katika Uwanja wa Bourg Al Arab uliopo jijini Alexandria. Taarifa iliyotolewa na Chama cha Mpira wa Miguu nchini Misri (EFA) imesema kuwa timu ya taifa ya nchi hiyo imezichagua Tanzania pamoja na Guinea kama timu zitakayopimana nazo nguvu kuelekea fainali hizo.

"Timu ya taifa ya Misri itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Tanzania, Juni 13 na dhidi ya Guinea, Juni 16 kwenye Uwanja wa Bourg Al Araba kabla ya kuanza kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON)," ilisema taarifa hiyo.

Misri ambao ni wenyeji wa mashindano hayo mwaka huu, wapo kundi A pamoja na timu za DR Congo, Uganda na Zimbabwe.

Tanzania yenyewe imepangwa kundi C pamoja na timu za Senegal, Algeria na Kenya. Timu mbili zitakazoongoza kundi zitafuzu hatua ya 16 Bora zikiungana na nne ambazo zina matokeo mazuri zitakazokuwa zimemaliza kwenye nafasi ya tatu