Stars, Zambia kuanza CHAN

Wednesday October 14 2020
CHAN PIC

TIMU ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ itaanza kutupa karata yake ya kwanza katika fainali za wachezaji wanaocheza soka la ndani (CHAN) Januari 19, 2021 dhidi ya Zambia mchezo utakaopigwa katika mji wa Buea, Cameroon.

Fainali hizo zinaanza rasmi mwakani, huku Tanzania wakiwa wamefuzu baada ya kuifunga Sudan 1-0 bao lililofungwa na Ditram Nchimbi kule Khartoum, nchini Sudan.

Stars watakuwa na kibarua kingine dhidi ya Namibia, Januari 23 mchezo utakaopigwa katika mji wa Buea saa 2:00 usiku huku mchezo wa mwisho ukipigwa dhidi ya Guinea katika mji wa Douala saa 2:00 usiku.

Fainali za kombe hilo zenye makundi manne zinatarajia kumalizika Februari 7 mchezo utakaopigwa katika jiji la Younde kwenye mji wa Ahmadou Ahidjo, Cameroon.

Timu zilizofuzu ni Cameroon, Zimbabwe, Mali, Burkina Faso, Libya, Niger, Dr Congo, Congo, Morocco, Togo, Rwanda, Uganda, Zambia, Tanzania, Guinea na Namibia.

Advertisement