Singida United kamili kuivaa Yanga

Muktasari:

Bingwa wa mashindano ya Kombe la FA atapata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani

Singida. Singida United imefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi kwenye Uwanja wa Namfua tayari kuwavaa Yanga katika mchezo wa robo fainali ya  kombe la FA utakaochezwa kesho Jumapili.

Katika mazoezi hayo, Singida United ilifanyia kazi namna ya upigaji wa mikwaju ya penalti kama watafika hatua hiyo kwenye mchezo wa kesho wasiwe na wakati mgumu.

Singida United itakuwa na faida kwenye mchezo huo kutokana na urejeo wa kipa wao namba moja, Peter Manyika Jr ambaye hata hivyo ameonekana kutokuwa fiti kwa asilimia zote.

Mara baada ya mazoezi hayo, kocha wa kikosi hicho, Hans van der Pluijm alisema licha ya kutokuwa na baadhi ya nyota wake wamejiandaa kushinda mchezo huo.