Simba yapiga tizi mwendo wa mashuti

Muktasari:

  • Simba inajianda kuivaa Yanga ikiwa na kumbukumbu ya ushindi mzuri dhidi ya mabingwa mara 8 wa Ligi ya Mabingwa Al Ahly

Dar es Salaam. Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesahau ushindi dhidi ya Al Ahly na leo asubuhi aliongoza mazoezi ya timu yake kwenye uwanja wa Boko Veterans kujianda na mechi dhidi ya Yanga.

Wachezaji wa Simba mara baada ya kufika katika uwanja wa Boko Veterans ambapo hufanya mazoezi walianza na mazoezi ya safa bwege.

Kocha Aussems aliugawa uwanja kwa kaweka goli dogo katika na kutaka kucheza timu mbili tofauti.

Kocha huyo alitaka kila timu icheze kwa pasi za haraka huku kufunga katika kila nafasi ambayo wataitengeneza

Mbali ya jua kuonekana kuwa kali, lakini nyota wa kikosi hiko walifanya mazoezi ya viungo huku wakiwa na furaha kwa kupiga shangwe la kushangilia.

Mara baada ya kumaliza mazoezi haya walifanya mazoezi yale ya kucheza huku wakiwa wamegawai timu mbili tofauti.

Timu ya kwanza ilikuwa na Dida, Wawa, Coulibaly, Dilunga, Ndemla, Rashid na Okwi.

Timu nyingine ilikuwa na Ally, Mkude, Mlipili Kagere, Salamba, Tshabalala na Niyonzima

Mashuti tu

Miongoni mwa mazoezi waliyofanya Simba ilikuwa ikifanya ni kupiga mashuti.

Kocha Aussema aliwaweka wachezaji Emmanuel Okwi, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Pascal Wawa, Rashid Juma na Zana Coulibaly wakipiga mashuti ya maana.

Goli kulikuwa na kipa Deo Munishi 'Dida' ambaye alikuwa akupangua mashuti hayo.

Kocha wa viungo wa Simba, Adel Zrane ndio aliwasimia wachezaji hao waliokuwa wakifanya mazoezi hayo.