Simba yamzawadia MO mabao 3-0 Taifa

Muktasari:

Kikosi cha Simba kimeendeleza ubabe baada ya kuwafunga Stand United mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara

Simba wanaendelea wimbi la ushindi baada ya kuwafunga Stand United mabao 3-0.
Mabao ya Simba yalifungwa na Cletus Chama aliyefunga bao la kwanza tangu alivyokuja nchini kujiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu.
Bao la pili lilifungwa na kinara wa mabao msimu uliopita Emmanuel Okwi ambaye anafunga mabao 20.
Huku Meddie Kagere nae alifunga bao la tatu ambalo lilikuwa la tano msimu na akiendelea moto wake wa kutupia.
Stand United wao walifanya mashambulizi ya kawaida na kushtukiza mara kadhaa na lakini wakashindwa kutumika nafasi hiyo.
Straika wa Stand United, Alex Kitenge ambaye aliwafunga Yanga mabao matatu katika mechi iliyochezwa uwanjani wa Taifa, ameshindwa kutamba.
Kitenge alipata nafasi moja tu kipindi cha kwanza ambayo alishindwa kutumia na mpaka mpira unaisha ilikuwa hivyo hivyo.