Simba yamvutia kasi beki Lipuli

Muktasari:

 Klabu ya Simba inatarajia kumsajili beki wa Lipuli ya Iringa Haruna Shamte kabla ya dirisha la usajili kufungwa leo saa sita usiku.

Dar es Salaam. Klabu ya Simba iko katika hatua za mwisho za kunasa saini ya mchezaji wake zamani Haruna Shamte akitokea Lipuli ya Iringa.

Usajili wa Shamte ni mapendekezo ya Kocha Patrick Aussems ambaye alisema anataka beki mpya kumsaidia Shomari Kapombe.

Kwa muda mrefu Kapombe amerejea katika mazoezi baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza jeraha la kifundo cha mguu.

"Tupo katika hatua za mwisho ya mazungumzo na Haruna Shamte na wakati wowote ataisaini mkataba wa kuitumikia klabu yetu," alisema kiongozi huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.

"Shamte bado hatujamsajili kama ikitokea tumemsajili tutamtangaza kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengine, lakini ambacho nafahamu tutafunga usajili kwa mchezaji wa maana mwenye uwezo zaidi ya waliokuwepo kama ambavyo kocha Aussems anataka,"alisema Magori.

Klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara ziko katika hatua za mwisho kukamilsia usajili wa wachezaji wao kabla ya dirisha kufungwa saa sita usiku leo.

&&&&&&&&