Simba yaitorosha Nkana

Muktasari:

Nkana baada ya kufahamu hilo walichukua maamuzi magumu ya kuhama na kwenda kujichimbia mahala ambapo, hawakutaka kufahamike hata na wanyeji wa hoteli ya Road View ambapo huwekaga kambi kila wanapokwenda kwenye mechi.

KABLA ya Simba kuwasili hapa Kitwe Zambia kikosi cha Nkana Rangers walikuwa wakiishi hoteli ya Road Porty View walihama fasta, ambapo huweka kambi kila wanapocheza mechi.
Ni kawaida Nkana kila wanapo kwenda kucheza mechi wakiwa hapa Zambia kuweka kambi hotelini hapo, Simba walipofika walichukua hoteli iliyokuwa karibu na kambi yao.
Hoteli waliochukua Simba Milford hadi walipokuwa Nkana hoteli ya Road Porty View ni umbali wa dakika tano tu.
Nkana baada ya kufahamu hilo walichukua maamuzi magumu ya kuhama na kwenda kujichimbia mahala ambapo, hawakutaka kufahamike hata na wanyeji wa hoteli ya Road View ambapo huwekaga kambi kila wanapokwenda kwenye mechi.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba Mlamu Ng'ambi, alisema hawakufahamu kuwa wamechukua hoteli ambayo ipo karibu na kambi ya Nkana.
"Tumepata tu taarifa kwamba wameondoka katika hoteli yao na kuhamia kwingine na baada ya hapo hatukutaka kufahamu lolote kuhusu wao," alisema Ng'ambi.
Nkana hawakuishia hapo kwani katika mkutano wa makocha kabla ya mechi hakuna kocha, nahodha wala kiongozi yoyote ambaye alitokea hapo.
Kocha wa Simba Patrick Aussems akiwa na Haruna Niyonzima, ambaye alikwenda kama nahodha walizungumza na mara baada ya kumaliza waliondoka.