Simba yaitandika Ruvu Shooting mabao 2-0 Taifa

Tuesday March 19 2019

 

By OLIPA ASSA

Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumanne leo usiku.

Vijana wa Kocha Patrick Aussems walipataa bao la kuongoza dakika ya 53 kupitia kwa nyota wake Paul Bukaba.

Dakika mbili tu baadaye Meddie Kagere aliongeza bao la pili kwa mkwaju wa penalti na kuifanya timu hiyo kuongoza kwa mabao 2-0 mechi ikiwa inaendelea Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Awali, wachezaji wasio na namba ndani ya kikosi cha kwanza cha Simba, walishindwa kumuonyesha kocha Aussems na msaidizi wake Denis Kitambi baada ya kuwaanzisha katika mechi ya leo na Ruvu Shooting kipindi cha kwanza.

Kuanzia kwa kipa tangu Ligi Kuu Bara ianze msimu huu, Aussems alikuwa anamchezesha Aishi Manula mchezo dhidi ya Ruvu alimuanzisha Deogratius Munishi 'Dida' ambaye muda mwingi ameonekana kujisahau kwa kutoka gorini mara kwa mra.

Safu ya mabeki Yusufu Mlipili, alianza akisaidiana na wanaocheza kikosi cha kwanza ambao ni Nicholas Gyan, Mohamed Hussein 'Tshabalala' na Paul Bukaba ambao kwa kiasi chake walijitahidi kuokoa hatari za hapa na pale.

Advertisement

Eneo la kiungo la Simba, likiongozwa na Jonas Mkude, Said Ndemla lilionekana kupambana zaidi dhidi ya wachezaji wa Ruvu Shooting ambao walionekata kutulia kuanzi safu yao ya ulinzi isipokuwa walikuwa hawana maarifa ya umaliziaji kwa mastraika wao kama Emmanuel Martin, Fully Zully na Hamis Ismail.

Washambuliaji wa Simba ambao walioanza kwenye mechi hiyo, wakiongozwa na Adam Salamba pamoja na  Mohamed Ibrahim, alianzisha mashambulizi ya pembeni wakati Ndemla na Dilunga wakicheza viungo ya juu lakini walipoozesha mpira mpaka kocha Aussems alipomtoa Dilunga na Juma dakika ya 43, nafasi zao zikichukuliwa na Meddie Kagere na Haruna Niyonzima.

Kuingia kwa Kagere na Niyonzima dakika ya 43 kumalizilia kipindi cha kwanza kuliichangamsha safu ya ushambuliaji wa timu hiyo ingawa haikuzaa matunda ndani ya kipindi cha kwanza.

 

Advertisement