Simba yaifuata Azam fainali

Friday January 11 2019

 

By Mwanahiba Richard

Mikwaju ya penalti ndiyo iliyoamua Simba kutinga fainali za Kombe la Mapinduzi ambapo watakutana na Azam FC.

Fainali hizo zitafanyika uwanja wa Amaan kisiwani Pemba ambako ndiko sherehe za Siku ya Mapinduzi Zanzibar zitafanyika.

Simba na Malindi zimelazimika kuingia kwenye mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 kumalizika bila kupatikana mbabe.

Simba imeshinda kwa penalti 3-1.

waliopata penalti upande wa Simba ni Yusuf Mlipili, Mohamed Ibrahim na Asante Kwasi huku Zana Coulibaly akikosa.

Upande wa Malindi aliyepata ni Abdulswamad Kasim wakati waliokosa ni Ali Juma, Muharami Issa na Cholo Ally.

Kocha wa Simba,  Nico Kiondo alifanya mabadiliko kwa kumtoa Yahaya Mbegu nafasi yake ilichukuliwa na Andrew Michael

Malindi nao waliwatoa Nasoro Juma, Haji Wahaji nafasi zao zilichukuliwa na Adeyun Saleh pamoja na Cholo Ally.

Advertisement