Simba yafunika tuzo Ligi Kuu

WACHEZAJI 15 kati ya 30 waliotangazwa kuwania tuzo mbalimbali kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20 wamepita hatua ya pili kabla ya Agosti 7, 2020 ambayo ni siku ya utoaji tuzo hizo kwenye Ukumbi wa Milimani City, jijini Dar es Salaam.

Kati ya wachezaji hao 15 waliopita kwenye mchujo huo nyota watatu kutoka Simba wamepenya ambao ni Cletous Chama, Luis Miquissone na Aishi Manula.

Katika kinya'anyiro cha Mchezaji Bora wamo Nicolas Wadada (Azam FC), Chama (Simba) na Bakari Mwamnyeto (Coastal Union).

Wanaowania kipengele cha goli bora ni Sadallah Lipangile KMC vs Mtibwa Sugar, Luis Simba vs Alliance FC na Patson Shikala Mbeya City vs JKT Tanzania.

Mchezaji Bora chipukizi ni Kelvin Kijiri (KMC FC), Dickosn Job (Mtibwa Sugar) na Novatus Dismas (Biashara United)

Kipa Bora ni Daniel Mgore (Biashara United), Nourdine Balora (Namungo FC) na Manula (Simba).

Timu yenye nidhamu ni Coastal Uniion, Kagera Sugara na Mwadui FC huku Mwamuzi Bora ni Ahmed Arajiga (Manyara), Ramadhan Kayoko (Dar es Salaam) na Abdallah Mwinyimkuu (Singida).

Mwamuzi Bora msaidizi ni Frank Komba (Dar es Salaam), Abdulaziz Ally (Arusha) na Hamdan Said (Mtwara).