Simba kupiga nne Sauzi

Muktasari:

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara Julai 27 dhidi ya Township Rollers ya Botswana ambao waliwatoa Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2018.

SIMBA wameweka kambi yao Afrika Kusini maalumu kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu bara na Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mashindano yote yanatarajia kuanza mwezi ujao.
Wakiwa huko, Simba watacheza mechi nne za kirafiki kabla ya kurejea nchini kuendelea na ratiba yao ya wiki ya Simba inayokwenda sambamba na sherehe zao za Simba Day inayofanyika kila mwaka August 8.
Mechi ya kwanza, Simba watacheza na Orbit Tvert itakayochezwa Julai 32, na siku moja baada ya mechi hiyo watacheza na Platinum Stars Julai 24.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara Julai 27 dhidi ya Township Rollers ya Botswana ambao waliwatoa Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2018.
Mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Afrika Kusini, Oralndo Pirates watacheza na Simba Julai 30 mwaka huu ambapo itakuwa mwisho wa mechi zao za kirafiki kabla hawajaanza safari ya kurejea nchini.