Simba hakuna kulala

Muktasari:

Kocha wa Simba Patrick Aussems mara baada ya kumalizika aliwatangazia nyota katika vyumba vya kubadilishia nguo kuwa kesho mazoezi Kama kawaida.

  Kocha wa Simba, Patrick Aussems mara baada ya kumalizika mchezo dhidi ya Stand United aliwatangazia nyota katika vyumba vya kubadilishia nguo kuwa kesho Jumatatu mazoezi kama kawaida.

Nyota wa Simba kwa nyakati tofauti siku moja mbele mara baada ya kucheza mechi hupewa mapumziko.
Kwa maana hiyo wachezaji wa Simba walitegemea mara baada ya kumaliza mechi na Stand United kesho watakuwa mapumziko.
Aussems amefuta mapumziko hayo ya siku moja baada ya mechi ya leo kwa kusema ratiba za mechi zipo karibu mno.
"Kweli nilikuta utaratibu wa kupumzika siku moja baada ya kucheza lakini kwa kuwa tunacheza mechi karibu kesho hakutakuwa na mapumziko, " alisema.
Kesho Simba wataendelea na mazoezi katika uwanjani wa Boko Veterans saa 10:00 jioni.