Simba, Mtibwa Sugar zatua pamoja

Muktasari:

Timu ya Simba inayowakilisha Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Mtibwa Sugar zitaanza kucheza mechi zao za raundi ya kwanza ugenini na itakuwa kati ya Desemba 13-14 na wa marudiano utakuwa kati ya Desemba 23-24.

Dar es Salaam. Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Simba na Kombe la Shirikisho Afrika Klabu ya Mtibwa Sugar, zimewasili pamoja jijini Dar es Salaam kwa tambo.

Simba ilikuwa Eswatini kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Mbabane Swallows ambayo wameing'oa katika mashindano hayo hatua ya awali kwa jumla ya mabao 8-1, na sasa imepita raundi ya kwanza na itacheza na Nkana Rangers ya Zambia.

Kikosi hicho kilitua na ndege ya Shirika la Afrika Kusini majira ya saa 9: 30 jioni muda mchache baada ya Mtibwa Sugar kuwasili na ndege ya Shirika la Emirates.

Mtibwa Sugar wao walikuwa wa kwanza na waliwasili saa 9:00, wakitokea Sherisheri walikokuwa na mchezo wao huo wa Kombe la Shirikisho ambapo sasa wanajiandaa nba mechi ya rauandi ya kwanza baada ya kuwatoa Northen Dynamo kwa jumla ya mabao 5-1.

Kikosi hicho, maarufu kwa jina la Wana Tamtam wao watakutana na KCCA ya Uganda mechi ya raundi ya kwanza.