Shughuli zasimama Iringa kisa Daimond

Saturday September 21 2019

 

By GODFREY KAHANGO, IRINGA

MSANII wa Bongo Flava, Nasib Abdul 'Diamond Plutnamz' na timu ya Wasafi amesimamisha kwa muda shughuli za maonyesho ya utalii karibu kusini baada ya kutinga katika viwanja vya Kihesakilolo kuangalia na kujifunza vivutio vilinavyotangazwa kwenye maonesho hayo.
Diamond amefika katika viwanja hivyo na kutembelea baadhi ya mabanda ya wawekezaji na kufika kwenye banda lao na kuwafanya mashabiki wake kumshangilia na baada ya kufika banda la wanyama na kumuona Simba wakaanza kumuita Simba kakutana na Simba mwenzake.
Watu waliokuwa kwenye viwanja hivyo wengi wao walisimamisha shughuli zao na kuanza kumfuatilia kwa nyuma na kutaka kupiga nae picha na wengine kumuona huku watoto wakimshangilia na kutaka apande jukwaani kuimba.
Diamond na timu yake baada ya kushuka kwenye basi lao umati wa watu walianza kumiminika na kuanza kumzonga wakitaka kupiga nae picha na wengine kumshika mkono.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alikuwa mwenyeji wa msanii huyo na timu yake ambapo alimuongoza kuzungukia mabanda ya maonesho kwa ajili ya kujifunza na kuangalia vitu vya kitalii vinavyooneshwa.
Muda wote alikokuwa akipita umati wa watu waliongia kwenye viwanja hivyo waliacha kufuata mambo yaliyowapeleka na kuanza kumfuata Diamond kila alikokuwa anakwenda huku wakiendelea kumzonga.
Hali ya utulivu ndani ya viwanja hivyo ilianza kutulia baada ya Diamond kuondoka na kuelekea Uwanja wa Somora kwa ajili ya kukagua maandalizi ya jukwaa la kufanyia muziki wake.
Diamond yupo mjini Iringa tangu Alhamis na usiku wa leo Jumamosi anatarajia kuwaburudisha wakazi wa Mjini Iringa katika ‘show’ ya Wasafi Festival katika Uwanja wa mpira wa Samora.

Advertisement