Shamte ni safi Simba

Muktasari:

Katika kipindi cha kwanza Shamte alikuwa akicheza kama beki wa kulia ambayo nafasi hiyo ndio amezoeleka kucheza lakini baada ya kwenda mapumziko alibadili namba na kwenda kucheza beki ya kushoto.

BEKI Haruna Shamte ameonyesha umahiri baada ya kucheza nafasi mbili uwanjani katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Bandari FC unaoendelea uwanja wa Taifa.

Kpindi cha kwanza Shamte alikuwa akicheza kama beki wa kulia nafasi ambayo amezoeleka kucheza lakini baada ya mapumziko alibadili namba na kwenda kucheza beki ya kushoto.

Katika kipindi hicho wakati kinaanza Simba ilimtoa chipukizi Joseph Peter aliyekuwa anacheza beki ya kushoto na kuingia Yusuph Mlipili, namba ambayo alienda kucheza Shamte.

Shamte katika beki ya kushoto alionekana kucheza kwa kujiamini kama ambavyo amezoeleka akicheza upande wa kulia.

Wakati huo huo Mlipili aliingia na kwenda kucheza beki ya kulia namba ambayo hajaozoeleka kucheza lakini bado alionyesha kupambana.

Mlipili ana kazi ya ziada kufanya kutokana eneo la beki wa kati kuna mabeki Pascal Wawa, Tairone Santos pamoja na Erasto Nyoni ambao wameonekana kuwa na uwezo.