Sebo naye kwenda Sauzi

Muktasari:

  • Azam imekuwa na utaratibu wa kuwapeleka nyota wake wenye matatizo kutibiwa nchini na kocha msaidizi wa klabu hiyo, Idd Nassor ‘Cheche’ alisema Sebo amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti na katika kuhakikisha anapata nafuu na kupona

NI suala la muda tu, ila beki wa Azam FC, Abdallah Kheri ‘Sebo’ anatarajiwa naye kupelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.

Taarifa ambazo Mwanaspoti limezinasa Hospitali ya Cape Town, Vincent Palloti na inaelezwa Sebo ataenda kutibiwa majeraha yake ya goti yanayomsumbua kwa muda.

Azam imekuwa na utaratibu wa kuwapeleka nyota wake wenye matatizo kutibiwa nchini na kocha msaidizi wa klabu hiyo, Idd Nassor ‘Cheche’ alisema Sebo amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti na katika kuhakikisha anapata nafuu na kupona.

“Kwenda Afrika Kusini umekuwa ni utaratibu wa timu kila mchezaji anapopata majeraha, ila taarifa kamili ya majibu ya huko au kinachoondelea kwa Sebo nadhani daktari wa timu ndio anafahamu zaidi,” alisema Cheche beki wa nyota wa zamani.

“Sebo amekuwa na kiwango kizuri ambacho kila siku kinazidi kuimarika na kufanya mpaka kuitwa katika timu ya taifa na kukosekana kwake hakutakuwa na mapungufu kwani katika nafasi yake kuna beki mwingine mzoefu atacheza ingawa kumkosa kwake si jambo jema kwa timu,” alisema Cheche.