Samatta kuiongoza Genk leo usiku

Saturday September 21 2019

 

By THOMAS NG'ITU

ACHANA na matokeo ya 6-2 waliyoyapata Genk dhidi ya Salzburg katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, kikosi hiko anachocheza mtanzania Mbwana Samatta leo kitashuka dimbani kucheza mchezo wa Ligi na KV Oostende katika uwanja wa Luminus Arena.
Genk katika mchezo huu wa Ligi, wanataka kuwafuta machozi mashabiki wao baada ya kupigwa kipigo kitakatifu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji Mbwana Samatta ndio nyota katika kikosi hiki baada ya kufunga magoli matano katika michezo sita aliyoichezea timu hii msimu huu katika Ligi Kuu.
Katika msimu huu wakiwa wamecheza michezo saba katika Ligi Genk wamecheza michezo mitatu nyumbani dhidi ya Anderlecht  na waliibuka na ushindi wa 1-0,2-1 Kortrijk wakifungwa 0-2 Zulte-Waregem .
Kwa matokeo ya ugenini Mechelen 3-1,  Waasland-Beveren 0-4, Club Brugge 1-1, Sporting Charleroi 2-1 Genk.

Advertisement