Salamba asahau yote Simba

Friday July 12 2019

 

By Olipa Assa

STRAIKA chipukizi wa Simba, Adam Salamba ameamua kusahau mambo ya nyuma aliyokumbana nayo msimu uliopita na kuanza kujipanga upya ili afanye mambo ndani ya klabu mpya iliyomsajili huko Sauzi.

Salamba aliyekuwa na wakati mgumu msimu uliopita kiasi cha kutokuwepo kwenye kikosi cha kwanza cha Kocha Aussems, alisema kuwepo kwake Msimbazi kumemfanya ajifunze mengi ikiwamo kusoma mazingira na sasa anajipanga upya kukipiga nje ya nchi.

“Mpaka nilipofika ipo hivi, nimekuwa nikijifunza changamoto za kila siku zinazonizunguka Simba, sikuwa na muda mzuri wa kucheza lakini nilijifunza uzoefu, ndivyo ilivyo kwenye timu ambayo nitaitumikia huku Sauzi,” alisema. Simba ilimsajili Salamba akitokea Lipuli ya Iringa, lakini hakuwa na nafasi ndani ya kikosi cha kwanza. Hata hivyo kapata zari la kuichezea TS Sporting ya Afrika Kusini.

Advertisement