VIDEO: Simba yaendelea kuiburuza Ruvu Shooting

Tuesday March 19 2019

 

By OLIPA ASSA

Ushindi wa Simba wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting jana Jumanne usiku umewafanya kupunguza uwiano wa pointi dhidi ya wapinzani wao Yanga ambao wapo kileleni kwenyemsimamo wa Ligi Kuu Bara.

Ushindi huo una maana ya kupunguza tofauti ya pointi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga ambao wanaongoza ligi kwa kumiliki pointi 67 katika mechi 28 walizocheza, wakishinda michezo 20 sare nne na wamepoteza mechi tatu.

Simba wamecheza 21 wameshinda mechi 17, wamefungwa mmoja na sare tatu kwa matokeo hayo wanaendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Simba kutokana na uwepo wa Kagere ambaye alionekana kuipa changamoto safu ya ulinzi ya Ruvu, Niyonzima akifanya kazi yake vyema eneo la kati.

Kutokana na mikiki mikiki ya Ruvu kushambuliwa gorini Simba walipata bao dakika ya 52 lililowekwa kambani na Paul Bukaba aliyepenyezewa pasi na Ndemla.

Dakika ya 54 Salamba alichezewa rafu na Tumba Sued ambae alilimwa kadi ya njano, huku Simba wakipewa penalti aliyopiga Kagere na wakafanikiwa kupata bao la pili. Mabadiliko aliyoyafanya kocha wa Simba, Aussems ya kumtoa Rashid na Dilunga na kumuingiza Kagere na Niyonzima yaliipa faida timu na yalibadilisha mchezo kuwa wa kasi.

Advertisement

Pia Mkude kipindi cha pili alirudi kucheza nyuma tofauti na cha kwanza ambapo alikuwa anapanda juu kufanya majukumu ya Dilunga ambaye alishindwa kuchezesha timu. Dakika ya 88 Hassan Dilunga alipeleka shambulizi kwa Simba kwa kuwapangua mabeki lakini Dida alidaka na kuutema ambapo Zully aliunganisha lakini mpira ulipaa juu.

Hata hivyo mabeki wa Ruvu waliokoa mashambulizi mengi ambayo yalikuwa yanaelekezwa kwa na washambuliaji wa Simba.

Advertisement