Rubby aanza mwaka kwa mkwara

Friday January 11 2019

 

By Rhobi Chacha

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ruby ameeleza kuwa yupo mbioni kuolewa.
Ruby ambaye kwa sasa anatamba na kibao kipya kinachoitwa Alele, ameliambia Mwanaspoti kuwa,ndoa yake iko karibu kwani taratibu zote  kabla ya kuona zishafanyika,kilichobaki ni ndoa tu.
"Nashukuru mwaka huu hautaisha nitakuwa nishafunga ndoa kwani hadi sasa tayari taratibu zote tukiwa wachumba na mchumba wangu zimeshafanyika ,kimebakia kipengelea cha ndoa tu,hivyo namshukuru mungu kwa hilo."
Hata hivyo Ruby amelitajia Mwanaspoti mpenzi wake anayejulikana kwa jina la 'Kusa' ambaye ni mwanamuziki na mwandishi wa nyimbo.

Advertisement