Prodyuza aliyemuibua Vanessa Mdee aaga dunia

Muktasari:

  • Pancho ndiye aliyemtambulisha msanii Vanessa Mdee katika ramani ya mziki wa Bongo Flava. Pia amefanya kazi mbalimbali za muziki wa Bongo Fleva ambazo zilibamba kwenye chati na kushika nafasi ya kwanza.

 MKALI wa kutengeneza biti za Mziki wa Bongo Flava, Pancho De Latino, amefariki dunia jana jioni baada ya kupata hitilafu ya maji alipokuwa katika kisiwa cha Mbudya kilichopo pembezoni mwa Daresalaam.

Pancho ndiye aliyegundua kipaji cha Vanessa Mdee kwa mara ya kwanza, baada ya kumkaribisha katika studio za B Hits na kufanya naye baadhi ya kazi ambazo zilimuweka msanii huyo katika ramani ya mziki.

Prodyuza huyu aliibuliwa na msanii mkongwe Dully Sykes katika studio za Dhahabu Records, lakini baadye alitimkia katika studio za B Hits akiwa chini ya wakongwe wa utengenezaji mziki Herm B.

Miongoni mwa nyimbo kali ambazo alizitengeneza karibu kwenye shoo za Joh (Joh Makini), Baadaye sana (Mabeste), Baby Candy (Dully Skyes), Usije Mjini (Mwana Fa ft Ay), Daresalaam Stand Up (Chid Benz),Mdananda (Sheta), Kariakoo ( Mataluma) na Bora Nikimbie (Linah).