Prisons yazindukia kwa Namungo

Saturday September 19 2020

 

By Oliver Albert

Baada ya kuanza  kuasua sua kwenye mechi mbili zilizopita za Ligi Kuu Bara, Prisons imezindukia kwa Namungo FC baada ya kuichapa bao 1-0  katika mchezo uliofanyiak kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Rukwa.

Wajela jela hao walianza Ligi kwa kutoka sare ya bao 1-1 na Yanga kabla ya kuchapwa na KMC mabao 2-1 hivyo mchezo wa leo ni wa kwanza kwao kuonja ladha ya ushindi tena wakiwa kwenye uwanja mpya.

Mchezo wa leo Jumamosi Prisons wamecheza kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Nelson Mandela Rukwa na kupata ushindi baada ya msimu huu kuamua kuukimbia uwanja wao wa Sokoine Mbeya.

Bao la Gasper Mwaipasi dakika ya 47 kwa shuti kali ndilo lililopeleka kilio  kwa Namungo Fc  ambayo mpaka sasa imecheza michezo mitatu na kuambulia pointi tatu.

Sasa Prisons itajiandaa kuikabili Azam katika mchezo utakaofanyika Septemba 26 kwenye Uwanja huo wakati Namungo itaikabili

 

Advertisement

Advertisement