VIDEO UCHAMBUZI: Presha juu! Timu 11 hazina uhakika kubaki Ligi Kuu

Wednesday May 15 2019

 

By Thobias Sebastian

LIGI Kuu Bara inaelekea ukingoni kwa mwisho wa mwezi Mei na kutambulika timu ambayo itachukua ubingwa ambayo itapata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika Ligi ya Mabingwa Afrika lakini zitatambulika timu tatu ambazo zitashuka kwenda Ligi daraja la kwanza msimu ujao huku Africana Lyon ikiwa imeshatangulia tayari kwani hata kama ikishinda michezo yote yoyote haiwezi kubadilisha matokeo.

Ukiondoa Simba waliokuwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi waliobakiwa na michezo mitano kabla ya msimu kumalizika timu nyingine zote zimebaki na michezo isiyozidi miwili mpaka mitatu.

Kutokana na msimamo wa ligi ulivyo timu ambazo nane ndio zinanafasi ya kubaki msimu ujao lakini nyingine zote hazipo nafasi salama na kama watashindwa kufanya vizuri katika michezo yao iliyobaki wanaweza kushuka na kwenda kucheza mechi za mitaoni na timu kutoka ligi daraja la kwanza na wakashindwa kufanya vizuri watashuka.

Timu nane ambazo zipo salama katika msimamo wa ligi na zimejihakikishia nafasi ya kuwepo msimu ujao Yanga ambao wanaongoza, Simba waliokuwa nafasi ya pili, Azam, KMC, Mtibwa Sugar, Lipuli, Ndanda na Singida United.

Kati ya hizo nane Yanga waliobakia na mechi mbili dhidi ya Mbeya City na Azam wanawania ubingwa dhidi ya Simba waliokuwa nafasi ya pili waliobakiwa na mechi tano dhidi ya Mtibwa, Ndanda, Singida, Biashara na Mtibwa kati hao timu hizo kongwe ambaye atamaliza vizuri mechi zake zilizobaki ndio atatatwaaa ubingwa na kuiwakilisha nchi katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Ukiachana na timu hizo nane ambazo zipo katika mahala salama kuna nyingine 11, ambazo mbali ya kubakiwa na michezo isiyozidi mitatu hawapo mahali salama kama watashindwa kufanya kufanya vizuri michezo yao iliyobaki kwa maana ya kupata ushindi zaidi ya kupoteza.

Advertisement

Katika msimamo kuanzia timu iliyokuwa nafasi ya tisa Coastal Union wenye pointi 44, hawapo mahali salama kwani Mwadui iliyokuwa nafasi ya 19, wakiwa na pointi 38, kama watashinda mechi zao mbili za mwisho watafikia pointi ambazo Coastal kama atashindwa kupata ushindi katika mechi tatu alizobaki nazo.

Timu 11, ambazo hazipo mahala salama na pointi zao kwenye mabano ni Coastal waliokuwaa nafasi ya tisa, Mbao (44), Mbeya City (43), Tanzania Prison (43), Kagera Sugar (43), Ruvu Shooting (42), Alliance (41), Stand United (41), JKT Tanzania (41), Biashara United (40), na Mwadui (38).

Advertisement