Pogba kuongezewa mkataba mpya

Manchester, England.Ole Gunnar Solskjaer amethibitisha kuwa klabu ya Manchester United ina mpango wa kumwongezea makataba wa mwaka mmoja kiungo Paul Pogba.

Mkataba wake wa sasa ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu bila kuwepo na mazungumzo yoyote yaliyotangazwa kwa ajili ya mkataba mpya.

Wiki iliyopita, kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa mara nyingine alidai kuwa na nia ya kujiunga na Real Madrid, akisema ni ndoto yake kuichezea miamba hiyo ya Hispania siku moja.

Lakini Solskjaer alisema: “Paul ni mchezaji wetu, atakuwa hapa kwa miaka mingine miwili na bila shaka atakuwa akijiandaa kuzidisha bidii na tunataka kuona akicheza katika kiwango cha juu.”

Solskjaer atakuwa akijiandaa kwa ajili ya kurudi vizuri kutokana na kutandikwa mabao 6-1 na Spurs katika mchezo wa Ligi Kuu England kabla ya kuivaa Newcastle Jumamosi.

Alisema: “Tunatakiuwa kurudi mchezoni haraka. Tunahitaji kujifunza baada ya kipigo kile.”