Pogba anaondoka Man United msimu huu

Wednesday May 15 2019

 

PAUL Pogba “ataondoka” Manchester United katika kipindi hiki cha usajili, amedai Mfaransa mwenzake Patrice Evra, huku pia beki huyo wa zamani akidai Alexis Sanchez alifuata pesa tu Old Trafford.

Evra anaamini tukio la mashabiki kumtukana Pogba, 26, ni ushahidi hapati mapenzi anayoyatarajia na atatimka msimu huu.

“Sitaki kuwalaumu wachezaji wote kwa sababu nafikiri kuna wachezaji hapa United na hawajui kwa nini wako hapa,” Evra aliiambia Sky Sports.

“Nadhani Pogba ataondoka, kwa sababu unatarajia kujihisi unapendwa unapocheza.

Evra aliongeza: “Baadhi ya wachezaji wamefuata pesa tu, Sanchez alikuwa na ofa pungufu Manchester City, akaacha kwenda kucheza soka zuri zaidi kule akaja United. Samahani kwa kusema, City wanacheza soka zuri zaidi.”

Pogba amekuwa na wakati mgumu United tangu enzi za Kocha Jose Mourinho na mara kadhaa imekuwa ikielezwa ataondoka kwenda Real Madrid.

Advertisement

Advertisement