Pogba ajumuishwa kutangaza jezi mpya Man United

Friday July 12 2019

 

PAUL Pogba amejumuishwa miongoni mwa wachezaji wa Manchester United walioteuliwa kutangaza jezi mpya za ugenini za klabu hiyo za msimu wa 2019-20 wa Ligi Kuu ya England.
Jezi hiyo mpya imebuniwa na adidas.
Pogba amejumuishwa miongoni wanaoitangaza jezi hiyo licha ya kuhusishwa na mipango ya kutaka kutimka Old Trafford katika kipindi hiki cha uhamisho.
Kiungo huyo Mfaransa ‘aliliamsha dude’  pale aliposema anataka kupata changamoto mpya mwingineko, na uvumi huo ukachochewa moto na wakala wake, Mino Raiola, aliposema kila mmoja klabuni hapo anafahamu kwamba Pogba anataka kuondoka na kwamba yeye anashuhughulikia uhamisho huo hivi sasa.
Real Madrid ndiyo inatajwa kuwa huenda Pogba anaelekea, lakini klabu hiyo inapaswa kwanza kumuuza Gareth Bale, Isco na James Rodriguez kabla ya kukamilisha dili hilo.
Juventus pia wanaripotiwa kutaka kumrejesha kikosini nyota wao huo wa zamani.

Advertisement