Oyaa wajumbe! Kwani Wolper anatuchukuliaje?

Friday August 14 2020

 

By KELVIN KAGAMBO

Hadi kufikia leo imetimia siku ya 5 tangu bosi wa lebo ya Konde Gang, Harmonize atoboe siri ya kwanini aliachana na aliyekuwa ‘My’ wake, mbongo movie Jackline Wolper; hiyo ni sawa na kusema hadi kufikia sasa zimeshatimia siku 5 bila Wolper kujibu tuhuma hizo kwa sababu hajapost chochote kuhusu ishu hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram, hajazungumza kwenye intavyuu yoyote na hata mwandishi wa gazeti hili alipompigia simu kumuuliza kuhusiana na kile kilichosemwa, alikata simu.

Kama stori hii ilikupita ni kwamba, Jumamosi wakati Harmonize akiwa kwenye shoo ya Jipoze jijini Dodoma alikuwa anajiandaa kuimba wimbo wa Niambie ambao katika video ya wimbo huo Wolper alicheza kama Video Queen. Sasa akiwa jukwaani, kabla ya kuanza kuimba, alikuwa anapiga stori na mashabiki wake waliojazana kwenye show hiyo na ndipo akawauliza; “Mnataka kujua kwanini niliachana na Wolper?”... mashabiki wakapiga “Ndiyoooo” na Harmonize akaanza kutiririka.

Kati ya mengi aliyoyasema, zilikuwemo tuhuma za kwamba huenda Wolper alikuwa akitoka kimapenzi na dogo dogo wake wa sasa, Rich Mitindo tangu kipindi akiwa kwenye uhusiano na Harmonize kwa sababu kwa mara kadhaa Harmonize amewahi kuona wakipostiana na mwanaume huyo kwa picha picha ambazo zimekaa kimahaba kimahaba.

Advertisement