Overmars anataka kazi Emirates

Muktasari:

  • Monchi na Unai Emery kocha wa Arsenal wanafahamiana vyema baada ya kuwa pamoja huko Sevilla ambako waliisaidia timu hiyo kushinda mataji matatu ya Europa League.

LONDON, ENGLAND.GWIJI wa Arsenal, Marc Overmars anataka kurudi kwenye timu hiyo kufanya kazi ya kuwa mkurugenzi wa ufundi mpya huko Emirates.

Overmars, 45, ambaye kwa sasa anafanya kazi kama hiyo huko Ajax, anataka kurudi zake kwenye Ligi Kuu England kuwa bosi kwenye kikosi cha Arsenal baada ya wababe hao kushindwa kumnasa Monchi.

Mwanzoni ilionekana kama Monchi, aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi huko kwenye kikosi cha AS Roma angekubali kwenda kuwa bosi Arsenal, lakini sasa mambo yamekuwa tofuati na huenda akatimkia zake Sevilla.

Monchi na Unai Emery kocha wa Arsenal wanafahamiana vyema baada ya kuwa pamoja huko Sevilla ambako waliisaidia timu hiyo kushinda mataji matatu ya Europa League.

Taarifa zinadai Monchi, 50, huenda akaiacha Arsenal hewani na kurudi zake Sevilla.

Arsenal imekuwa ikisaka mkurugenzi wa ufundi mpya ili kuziba pengo lililoachwa wazi na Sven Mislintat, ambaye aliacha kazi Novemba mwaka jana. Overmars aliwahi kukipiga kwenye kikosi cha Arsenal kwa miaka mitatu kati ya mwaka 1997 na 2000 kabla ya kutimkia zake Barcelona na sasa anataka kurudi klabuni hapo akiwa bosi.