Nyundo 15 za JPM kwa Stars

Muktasari:

  • Hapa ni maswali magumu 15 yanayoweza kuwapasua vichwa watendaji hao, walioalikwa Ikulu sanjari na wachezaji wa Stars ambao walipata ‘lunch’ na Rais.

RAIS John Magufuli ameshusha nyundo kali kwa watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na wale wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), kuhusiana na mambo yalivyo kwenye sekta ya michezo.

Jana, wakati akiwapongeza wachezaji wa Taifa Stars kwa kufuzu Fainali za Afrika (Afcon), sambamba na bondia Hassan Mwakinyo, Rais Magufuli aliamua kuwachana hadharani vigogo hao huku akihoji maswali magumu.

Hapa ni maswali magumu 15 yanayoweza kuwapasua vichwa watendaji hao, walioalikwa Ikulu sanjari na wachezaji wa Stars ambao walipata ‘lunch’ na Rais.

1)Nilikuwa najiuliza katika mechi na Lesotho wachezaji wazuri hawakupangwa ama mwalimu aliingiliwa majukumu yake. Stars ililala bao 1-0.

2)Taifa la watu milioni 55 tunafungwaje na watu milioni 2, yaani tumeshindwa kupata wachezaji 11 wazuri wa kuwafunga Lesotho?

3)Uwanja wa Taifa unachukua watu 60,000, lakini jana (juzi) mlikata tiketi zaidi ya 63,000 na mashabiki wengi walikuwa nje na tiketi, hizi hela nyingine zinakwenda wapi.

4) Hivi asilimia za malipo ya fedha za uwanja zinatumika kufanya nini?

5 )|Uwanjani mambo mengi hayaendi vizuri, wizara inataka iundiwe kamati kusimamia hilo?

6)Tiketi za Tanzania huwa hazina ukomo na hivi Wizara inaangalia usalama wa mashabiki?

7)Kama uwanja ungeanguka ni watu wangapi wangepoteza maisha?

8)Fedha ambazo zimeanza kuja nchini kupitia TFF, hivi tunajipanga katika kuweka uwazi wa matumizi yake ili kuleta tija?

9)Makusanyo ya viingilio tunayopata yana tija gani kwa wachezaji, hawa wananufaika na jasho lao?

10) Hivi ni kwanini Taifa Stars imeshindwa kufuzu Afcon kwa miaka 39?

11) Kwanini enzi za Mwalimu Nyerere tulifuzu Afcon

12) Wanariadha wetu wanapokwenda nje kwanini hawafanyi kama kina Filbert Bayi?

13) Kwanini timu za ngumi zilihusika katika dawa za kulevya nje ya nchi?

14) Kwanini inapocheza Simba, Yanga hawaipi sapoti kuonyesha uzalendo?

15) Hivi viongozi wa wizara hawaendaji uwanjani kuangalia maendeleo yake?