Nyota wa Simba Queens kupitishiwa mchujo

Muktasari:

  • Kocha wa Simba B, Mussa Hassan Mgosi alisema anaamini timu hiyo ikiongeza juhudi zaidi wanaweza wakachukua taji la ubingwa msimu huu.

Kocha wa Simba Queens, Omary Mbweze amesema kitu kikubwa anachotarajia kukifanya baada ya kumalizika kwa raundi ya kwanza ni tathimini ya mchezaji mmoja mmoja namna alivyochangia timu.
Mbweze alisema kila mchezaji ndani ya kikosi chake anajua nini kimempeleka Simba Queens, huku akisisitiza kujitathimini mpaka sasa mchango wao ni asilimia ngapi.
“Kiufundi wanaelekea kwenye malengo yetu ambayo ni kuchukua ubingwa kwa msimu huu, hivyo lazima tuwe tunawakumbusha kila wakati mpaka mwisho.
“Nawapongeza lakini sina maana tumeridhika, kuna timu tunashindana nazo kwenye nafasi za juu kama JKT Queens ambayo haijapoteza mechi hata moja, kwetu ni funzo la kuongeza nguvu zaidi.”
Kocha wa Simba B, Mussa Hassan Mgosi alisema anaamini timu hiyo ikiongeza juhudi zaidi wanaweza wakachukua taji la ubingwa msimu huu.
“Waongeze nguvu, wachukukilie kwa uzito majukumu yao hilo litawafanywa wawe wa todauti dhidi ya wapinzani wao, wasiogope timu iliopo keleleni wao wapambane tu,” alisema.