Kinda azitesa Simba, Yanga msimu huu

Thursday December 7 2017

 

By ELIYA SOLOMON

UMUHIMU wa kuwepo kwa matangazo ya moja kwa moja ya soka  ni mkubwa kwa hata wachezaji wa Ligi Kuu Bara na  hiyo kumbe ndiyo siri ya Eliuter Mpepo wa Tanzania Prisons kuzitesa Simba na Yanga.
Mpepo ambaye staili yake ya uchezaji inahusisha nguvu nyingi amejipatia umaarufu baada ya kuisumbua ngome ya ulinzi ya Simba kabla ya kuja kuifunga Yanga kwenye mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya  bao 1-1.
Huu ni msimu wa kwanza kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kucheza Ligi Kuu akitokea Mbeya Kwanza ambayo inashiriki daraja la kwanza, mpaka sasa Mpepo ameifungia timu yake mabao 3 ndani ya michezo 7.
Hata hivyo mshambuliaji huyo alimtaja Athuman Mchupa kama mshambuliaji wake ambaye alikuwa akimhusudu na  kujifunza  mengi wakati akianza safari yake ya kucheza soka.