Nyoni: Ahsanteni Watanzania

Muktasari:

  • Nyoni alisema: “Namshukuru Mungu tulijiandaa vizuri na hadi siku ya mechi yenyewe na kupata ushindi kikubwa ni kuzingatia yale maelezo tunayoambiwa na makocha ikiwemo kujituma pamoja na ushirikiano wa wachezaji na Watanzania ulikuwa mkubwa.

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) wakishika nafasi ya pili kundi D kwa kukusanya pointi nane nyuma ya Uganda wenye pointi 13. Kufuzu kwa Stars ni baada ya kuifunga Uganda bao 3-0 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao hayo matatu yalifungwa na Saimon Msuva, Aggrey Morris na Erasto Nyoni katika mchezo huo.

Nyoni alisema: “Namshukuru Mungu tulijiandaa vizuri na hadi siku ya mechi yenyewe na kupata ushindi kikubwa ni kuzingatia yale maelezo tunayoambiwa na makocha ikiwemo kujituma pamoja na ushirikiano wa wachezaji na Watanzania ulikuwa mkubwa.

“Shukrani za pekee ziende kwa Rais wa nchi yetu Dk. John Magufuli amekuwa mlezi na Baba yetu ambaye anatusaidia kwa hali na mali na tulimpa ahadi ya kufuzu kwani alituchangia Sh 50 milioni ili tuhakikishe tunafuzu na tumetimiza ahadi.”