Nyie! Arsenal wataka Emery afukuzwe kazi

Saturday June 8 2019

 

LONDON, ENGLAND.ARSENAL imeshasikia chokochoko za mastaa wake Alexandre Lacazette na Pierre-Emerick Aubameyang kuwindwa na timu nyingine, hivyo wameanza mchakato mapema wa kusaka mtu wa kuja kuziba pengo lao na mabao yakaendelea kupatikana.

Kikosi hicho cha kocha Unai Emery kimeanzisha mpango wa kwenda kumsajili staa wa CSKA Moscow, Fedor Chalov, ambaye ni kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu Russia, ambaye anasakwa pia na vigogo Monaco na Sevilla.

Kocha Emery anajaribu kusaka wachezaji wakali kwa kuzingatia bajeti yake ya Pauni 40 milioni, licha ya kwamba anaamini ataingiza mkwanja mrefu zaidi kama mastraika wake matata Aubameyang na Lacazette wataamua kuondoka.

Chalov ni bonge la staa huku akiwa bado mdogo kabisa, miaka 21 tu, akifunga mabao 15 katika mechi 30 alizocheza msimu huu na aliwafunga Arsenal kwenye robo fainali ya Europa League.

Alifunga bao pia kwenye ushindi wa 3-0 iliyoupata CSKA dhidi ya Real Madrid huko Bernabeu, hivyo Emery anaamini kuwa na huduma ya straika huyo haiwezi kuwa shida sana kama wakali wake Aubameyang na Lacazette wataondoka.

Kocha Emery angekuwa na pesa nyingi za kusajili, zaidi ya Pauni 100 milioni kama chama lake lingefuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, lakini kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwe Chelsea kwenye fainali ya Europa League na kumaliza Ligi Kuu England nje ya Top 4 kimetibua mpango huo.

Advertisement

Advertisement