Niyonzima: Luis ni fundi kwelikweli

Muktasari:

Kipa wa Lipuli ya Iringa, Deogratius Munishi ‘Dida’ alisema; “Kwa uwezo aliouonyesha kwenye mechi alizocheza ana kipaji kikubwa, anajitolea kupambana binafsi hata kama timu inacheza chini ya kiwango, ataisaidia Simba.”

LICHA ya winga wa Simba, Luis José Muquissone kutamka kuwa bado hajacheza kwenye kiwango chake, Haruna Niyonzima wa Yanga na wachezaji wengine wamekubali ubora wake.

Beki wa zamani wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambaye amekwenda kucheza soka Latvia alisema; “Nikizungumzia kiufundi yule jamaa anaujua mpira, ndio maana unakuta alikuwa anakabwa na watu watatu ili mradi kumpunguza kasi asifike golini kwa Yanga, ndiye mtu niliyemuona hatari zaidi kwa lango lao.”

“Hakuna mchezaji hatari kama anayechezea miguu miwili halafu nafasi ya mbele, unakuwa hujui anaamua nini na kwa wakati gani, binafsi naona Simba imesajili kifaa,”alisema.

Ukiachana na alichosema Ninja, Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima alisema Muquissone; “Kila mchezaji ana ubora wake, naona analazimisha sana mipira iende mbele, ana nguvu naamini ndio maana timu yake imemsajili.”