Neymar ahojiwa polisi saa tano

Muktasari:

Mwanamke anayedaiwa kubakwa alishahojiwa na polisi hao wa Brazil mwezi uliopita.

SAO PAULO, BRAZIL.SUPASTAA Neymar ametumia saa tano katika kituo cha polisi akihojiwa kuhusiana na tuhuma za ubakaji zinazomkabili dhidi yake.

Staa wa Kibrazili alisema ukweli utafahamika tu kama sio sasa basi baadaye wakati alipokuwa akitoka kwenye kituo hicho cha polisi huko Sao Paulo, Brazil, juzi Alhamisi jioni.

Neymar ambaye ni staa wa PSG ya Ufaransa alivaa suti nyeusi huku akitembea kwa msaada wa magongo baada ya kuumia enka hivi karibuni, kwenye kituo hicho cha polisi aliandamana na wanasheria wake.

Mwanamke anayedaiwa kubakwa alishahojiwa na polisi hao wa Brazil mwezi uliopita.

Mashabiki bado wanaonekana kumkubali Neymar licha ya tukio hilo ambalo wengi walionekana wakimshangilia wakati alipokuwa akiingia kwenye kituo hicho cha polisi.