Kipa wa Simba kutua leo nchini

Muktasari:

  • Kipa huyo alikwenda kutibiwa nje ya nchi na anatarajiwa kujiunga na wenzake lakini akianzishiwa program maalumu ya mazoezi.

KIPA wa Simba, Said Mohamed Nduda anatarajia kuwasili nchini leo Jumatatu akitokea India kwa matibabu  lakini bahari njema kwa mashabiki wake ni kwamba, atarudi uwanjani rasmi, mapema Januari.

Nduda ambaye kwa sasa alikwenda India mwanzoni mwa mwezi huu kwa ajili ya upasuaji wa goti, ameshatibiwa na anarudi akiwa tayari ameshaanza programu maalumu ya azoezi ya viungo.

Amesema: "Namshuku Mungu nawashukuru Simba na wadau wote wa michezo kwa kufanikisha hili, ninachoomba ni kurudi katika afya yangu. Nimepewa programu maalumu ya mazoezi ya viungo ambayo nilianza baada ya kutibiwa na mazoezi ya uwanjani, nimeambiwa mpaka baada ya miezi miwili."

Mchezaji huyo alipata maumivu ya goti Kisiwani Zanzibar alipokuwa na kikosi chake katika maandalizi ya msimu wa ligi na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.