Mwasapili ajipanga upya Azam FC

Wednesday June 12 2019

 

By Charity James

Dar es Salaam. Beki wa Azam FC, Hassan Mwasapili amesema hakuwa na msimu mzuri tangu amejiunga na matajili wa Chamanzi.

Mwasapili alijiunga na Azam FC akitokea Mbeya City akiwa mchezaji wa kikosi cha kwanza, lakini ameshindwa kuonyesha ubora wake na mabingwa hao wa Kombe la FA.

Mwasapili alisema katika soka jambo kama alilokutana nalo ni kawaida kikubwa nachokiangalia kwa msimu ujao ni kuhakikisha napambana kupata namba kikosi cha kwanza ili aweze kurudisha makali yake ya ushindani.

"Bado nipo Azam FC ni mchezaji sionekani kwa sababu sipati nafasi, lakini naamini muda utaongea nimejipanga kuhakikisha napata namba kikosi cha kwanza ili kurudisha jina langu kwa mashabiki ikiwa ni pamoja na kupambani nafasi kikosi cha timu ya taifa."

"Nilijiunga na Azam nikitokea Mbeya City ambayo nilikuwa mchezaji tegemezi na niliondoka kuja huku kujaribu changamoto nyingine, lakini imekuwa tofauti ni moja ya changamoto katika soka sijakata tamaa nitapambana kuhakikisha narudisha heshima yangu," alisema Mwasapili.

Advertisement