Mwanaspoti yazidi kumwaga zawadi

Friday July 19 2019

 

By Thobias Sebastian

WASHINDI sita wa Shinda Mchongo wa Mwanaspoti walipatikana jana Ijumaa, katika droo ya pili iliyofanyika katika studio za Azam Media zilizopo Tabata T.O.T, jijini Dar es Salaam.
Washindi hao wameshinda zawadi tofauti ambapo watano wa kwanza walipata Sh 100,000 kila mmoja na mshindi wa sita alipata zawadi ya simu za kisasa (Smartphone).
Mshindi wa smartphone ni Abdud Kipanda kutoka Mbeya, washindi wengine watano wa Sh 100,000  ni Joseph Mwasumbi kutokea Mbeya, Hamza Juma wa Tandika na Dinah Edward Kigogo wote wa Dar es Salaam, Hamza Juma, Shabani Bakly wa Mkuranga Pwani na Phares Mgongo wa Kibaha Pwani.
Washindi hao watapatiwa zawadi zao na Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwanaspoti, Mwananchi na The Citezens.
Katika hatua nyingine droo ya tatu itachezwa wiki ijayo itatolewa mshindi wa pikipiki (bodaboda), na zawadi kubwa kuliko itatolewa mwisho wa droo ambayo itakuwa Sh 10, milioni.

Advertisement