Manyika ajifungwa mwaka Polisi Tanzania

Tuesday January 14 2020

Mwanaspoti-Manyika-Tanzania-Mwanasport-ajifungwa-mwaka-Polisi Tanzania-Michezo

 

By THOMAS NG’ITU

Dar es Salaam.Kipa Peter Manyika amejiunga na Polisi Tanzania kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea KBC ya Kenya.

Manyika amejiunga na Polisi Tanzania inayonolewa na Malale Hamsini baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na KBC.

Akiwa KBC kipa huyo hakuweza kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza na ilielezwa pia ukata unaoendelea katika Ligi hiyo ulimfanya arejee nchini kimya kimya mpaka mkataba wake unaisha.

Usajili huu unaongeza chachu ya namba katika kikosi cha Polisi Tanzania kwani pale kuna Mohamed Yusuph ambaye aliwahi kujumuishwa katika kikosi cha Stars.

Manyika aliibukia Simba na baadaye alienda Singida United kisha akatimkia zake KBC nchini Kenya.

Advertisement