VIDEO: Kakolanya: Nilijua katika penalti tano moja lazima

Muktasari:

Kipa huyo alicheza penalti ya mwisho iliyoipeleka Simba fainali ikipigwa na kipa mwenzake wa Azam, Razack Abalora na kuifanya Simba kushinda kwa penalti 3-2.

Zanzibar. Kipa wa Simba, Benno Kakolanya amesema hatua ya kucheza kwake penalti na kuisaidia timu yake kutinga fainali wala hakujamshtua.

Kakolanya amesema baada ya kumaliza dakika 90 katika mchezo wa jana dhidi ya Azam huku matokeo kuwa suluhu hakuwa na wasiwasi.

Kipa huyo amesema alijua kwamba katika penati tano za Azam isingekuwa rahisi kwake kama angeshindwa kucheza penalti moja au mbili.

Amesema licha ya kupata mazoezi ya mikwaju ya penalti lakini ana ubora mzuri wa kucheza mipira hiyo.

Aidha kipa huyo ameongeza kuwa kwasasa wanajipanga katika mchezo mwingine mgumu wa fainali dhidi ya Mtibwa Sugar na kwamba wanatambua hautakuwa rahisi.

Kipa huyo alicheza penalti ya mwisho iliyoipeleka Simba fainali ikipigwa na kipa mwenzake wa Azam, Razack Abalora na kuifanya Simba kushinda kwa penalti 3-2.