VIDEO: Hukumu ya Malinzi yaanza kusomwa mahakamani Kisutu

Wednesday December 11 2019

Mwanaspoti-Hukumu-Malinzi-Tanzania-yaanza-kusomwa-mahakamani-Kisutu

 

By Khadija Jumanne

Dar es Salaam.Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeanza kusoma hukumu dhidi ya aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake watatu.

Hukumu hiyo imeanza kusomewa mchana huu na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Maira Kasonde.

Mbali na Malinzi, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa; Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, na Karani Flora Rauya.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha.

Itakumbukwa kuwa, Julai 23, 2019, mahakama hiyo, iliwakuta na kesi ya kujibu.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii.

Advertisement

Advertisement